• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hekaheka za Afcon sare za 1-1 zatawala katika mechi za kundi D

    (GMT+08:00) 2015-01-21 15:59:41

    Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Iliendelea kutimua vumbi jana nchini Guinea ya Ikweta, ambapo timu za kundi D zilichuana kuwania pointi tatu muhimu. Katika mechi hizo Ivory Coast imejikuta ikotoka sare ya moja kwa moja dhidi ya Guinea baada ya Guinea kuwa wa kwanza kupata bao licha ya mshambuliaji Gervinho kupewa kadi nyekundu. Guinea ilianza kuongoza mnamo dakika ya 36 baada ya Mohammed Yattara kuchana wavu. Aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal Gervinho ambaye mkwaju wake ulipiga mwamba wa goli la Guinea katika kipindi cha kwanza alipewa kadi nyekundu na hivyo basi kutoka nje katika dakika ya 58. Mchezaji Traore wa Guinea karibia apate bao la pili wakati kombora lake lilipogonga mwamba wa goli, lakini Ivory Coast ilijiokoa baada ya Seydou Doumbia Kufunga katika eneo la hatari. Kwa upande wa Mali na Cameroon pia zilitoka sare ya 1-1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako