• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Suprise" yamtoa jino Tiger Wood

    (GMT+08:00) 2015-01-21 16:01:17

    Mchezaji nguli wa zamani wa mchezo wa gofu Tiger wood amepoteza jino lake la mbele la juu baada ya kugongwa na kamera wakati akimtazama mpenzi wake Lindsey Vonn akinyakua kikombe cha ushindi. Tiger wood aliamua kwenda katika michuano ya kuteleza kwenye barafu ili kumshangaza Vonn mpenziwe ambaye alikuwa hamtarajii kumwona akichuana Cortina d'Ampezzo huko Italia. Balaa hilo lilimkumba baada ya kwisha kwa michuano hiyo ya kuteleza barafuni, ambapo watu walijisogeza karibu na mimbari ya kutolea tuzo, ili kupata picha nzuri huku wakisukumana, mwandishi mmoja aliposukumwa na mwenziwe kiasi cha kuteleza kutoka mimbarini na kamera kumtoka na kumgonga Tiger Woods mdomoni, na wakala ya nguli huyo wa zamani wa mchezo wa gofu alieleza hali hiyo kuwa aligongwa kwa bahati mbaya

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako