• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa China kutoshuka kwa kiasi kikubwa

    (GMT+08:00) 2015-01-22 11:02:26

    Waziri Mkuu wa China Bw Li Keqiang amesema uchumi wa China hautashuka kwa kiasi kikubwa.

    Katika hotuba aliyotoa kwenye mkutano wa baraza la uchumi wa dunia, Bw Li amesema uchumi wa China umeingia kwenye hali mpya ya kawaida, na kupungua kidogo kwa kasi ya ongezeko la uchumi wa China kunaendana na mabadiliko makubwa yaliyotokea katika uchumi wa dunia. Bw Li amesema China itaendelea kutekeleza sera ili kutuliza ongezeko la uchumi.

    Katika mkutano huo Bw Li pia alikutana na Rais Petro Poroshenko wa Ukraine na kuzungumzia hali ya Ukraine, Bw Li amesema China inaunga mkono kutatua mgogoro wa Ukraine kwa njia ya mazungumzo na itaendelea kutoa mchango kufanikisha juhudi hizo. Pia amesema China inafuata msimamo usio wa upendeleo kuhusu mgogoro wa Ukraine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako