• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yasema ina wasiwasi na vita dhidi ya Ebola Afrika magharibi

    (GMT+08:00) 2015-01-24 17:54:56

    Shirika la Afya Duniani WHO limesema lina wasiwasi na vita dhidi ya Ebola Afrika magharibi licha ya kupungua kwa visa vya maambukizi katika eneo hilo.

    WHO imesema hayo saa chache tu baada ya Sierra Leone kutangaza kuondoa kabisa vizuizi vya kuzuia maambukizi ya Ebola kote nchini humo. Akizungumza na waandishi wa habari, mkurugenzi mkuu msaidizi wa WHO Bw. Bruce Aylward amesema kwa wiki kadhaa sasa kasi ya maambukizi mapya ya Ebola yamepungua katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone. Hata hivyo Bw Bruce amesema mapambano dhidi ya Ebola yanakabiliwa na upungufu wa dola za kimarekani milioni 350 pamoja na wafanyakazi wa matibabu. Bruce pia amesema majira ya mvua pia huenda yakaleta changamoto kubwa kwa mapambano hayo.

    Habari zaidi zinasema , balozi wa China nchini Sierra Leone Bw. Zhao Yanbo amesema, China haitasitisha uungaji wake mkono kwa Sierra Leone hadi ugonjwa wa Ebola utokapotokomezwa kabisa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako