• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia Afrika magharibi kupambana na Ebola

    (GMT+08:00) 2015-01-26 20:55:16

    Shirika la Afya Duniani WHO limesema, mlipuko mkali wa Ebola umeonesha udhaifu wa mfumo wa afya katika nchi za Afrika magharibi, pamoja na uwezo mdogo wa shirika hilo wa kukabiliana na Ebola.

    Akizungumza kwenye mkutano maalum kuhusu Ebola mjini Geneva, mkurugenzi mkuu wa WHO Bibi Margaret Chan amesema, ingawa kasi ya maambukizi mapya ya Ebola imepungua, lakini bado haijafikia lengo la kutokomeza kabisa ugonjwa huo. Ameitaka jumuiya ya kimataifa ifanye juhudi kukomesha maambukizi ya Ebola mapema iwezekanavyo, kuuunga mkono ujenzi wa mfumo wa afya wa nchi za Afrika, na kuliunga mkono shirika hilo kukamilisha utaratibu wa kukabiliana na matukio ya dharura.

    Katika mkutano huo, China imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuimarisha ushirikiano chini ya utaratibu wa Umoja wa Mataifa na WHO, kusaidia Afrika magharibi kupambana na maambukizi ya Ebola, na kujenga upya mfumo wa afya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako