• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Juventus huenda ikampoteza mchezaji Paul Pogba

    (GMT+08:00) 2015-01-27 14:09:08
    Kocha wa klabu ya Juventus Masimiliano Allegri amechochea tetesi za kuondoka kwa nyota wake Paul Pogba baada ya kuwataka mashabiki wa klabu hiyo kumtazama Pogba kwa kipindi hiki wakati akiwa Juventus kwani huenda wasipate nafasi hiyo tena. Pogba mwishoni mwa wiki iliyopita alifunga bao moja huku akisaidia kutengeneza bao jingine katika mechi ya Juventus dhidi ya Chievo Veron mechi ambayo Juve walishinda 2-0 ukiwa muendelezo wa kiwango bora ambacho ameendelea kukionyesha tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea Manchester United. Tetesi mbalimbali zimemhusisha Pogba na kujiunga na klabu kadhaa barani ulaya zikiwemo Paris St Germain, Real Madrid, Manchester City, Chelsea na Manchester United ambazo kwa nyakati tofauti zimehusishwa na nyota huyo. Pogba mwenyewe ameonekana kuziongeza kasi tetesi hizi baada ya kusema kuwa angependa kurudi Manchester United huku kwa wakati mwingine akisema kuwa ameanza kujifunza lugha ya kihispania ambapo kauli hiyo imehusishwa na mpango wa kujiunga na mabingwa wa ulaya .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako