• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Poland yaadhimisha miaka 70 ya kambi ya Auschwitz

    (GMT+08:00) 2015-01-28 10:58:47

    Jana ilikuwa ni siku ya kimataifa ya kuwakumbuka watu waliouawa kwenye mauaji ya halaiki ya wayahudi. Nchini Poland siku hiyo iliadhimishwa kwa kukumbuka miaka 70 ya ukombozi wa kambi ya Auschwitz, shughuli iliyohudhuriwa na watu 300 walionusurika kwenye mauaji ya halaiki ya wayahudi katika kambi hiyo, na wawakilishi kutoka karibu nchi 50.

    Rais Bronislav wa Poland na wahanga wengine waliweka maua kwenye ukuta wa mauaji. Marais kutoka Ujerumani, Ukraine, Ufaransa na Lithuania, na wawakilishi kutoka nchi nyingine nyingi pia walihudhuria shughuli hiyo.

    Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku hiyo, katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Bw Ban Ki-moon ametoa mwito wa kuondoa msingi wa chuki na kutokuwa na uvumilivu. Na Rais Joachim Gauck wa Ujerumani pia alionya kutosahau historia ya mauaji hayo kwa Ujerumani, na kutoka mwito wa kuishi kwa masikilizano kwa tamaduni na dini mbalimbali nchini Ujerumani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako