• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watumiaji wa mtandao wa 4G nchini China yazidi milioni 97

    (GMT+08:00) 2015-01-28 18:50:22

    Wizara ya viwanda na teknolojia ya habari ya China imesema, mwaka jana mchango wa matumizi katika teknolojia ya habari ulikuwa mkubwa, sekta ya mawasiliano ya simu ilikua kwa utulivu, biashara ya mtandao wa internet wa 4G iliendelea vizuri kuliko ilivyotarajiwa, na idadi ya watumiaji wa mtandao wa internet wa 4G imefikia milioni 97.28.

    Takwimu zilizotolewa na wizara hiyo zinaonesha kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, idadi ya watumiaji wa mtandao wa mobile internet nchini China ilikuwa milioni 583, thamani ya biashara kwenye mtandao wa internet ilifikia dola za kimarekani trilioni 1.9. Pia thamani ya biashara ya software ilikuwa dola za kimarekani bilioni 590, na thamani ya jumla ya matumizi katika sekta ya teknolojia ya habari ilifikia dola za kimarekani bilioni 448.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako