• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makamu wa rais wa China ashiriki kwenye mazungumzo ya tatu kati ya vyama tawala vya China na Sudan

    (GMT+08:00) 2015-01-28 19:57:24

    Makamu wa rais wa China Bw. Li Yuanchao amehudhuria mazungumzo ya tatu ya ngazi ya juu kati ya vyama tawala vya China na Sudan.

    Ujumbe wa chama tawala cha NCP cha Sudan umeongozwa na naibu mwenyekiti wa chama hicho Bw. Ibrahim Ahmed Ghandour ambaye pia ni msaidizi wa rais wa Sudan.

    Akitoa hotuba kwenye mazungumzo hayo yaliyofanyika leo hapa Beijing, Bw. Li amesema, China kamwe haitabadili sera ya kuendeleza urafiki kati ya chama na serikali yake na Sudan. Naye Bw. Ghandour amesema, Sudan inathamini urafiki wa jadi kati yake na China na inapenda kutumia mazungumzo hayo yaliyofanyika kati ya vyama hivyo viwili kuongeza mawasiliano na uratibu katika utawala wa nchi.

    Wakati huohuo, mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China Yu Zhengsheng amesema, licha ya mabadiliko katika mazingira ya kimataifa, Sudan na China zimedumisha uaminifu wa kisiasa na mawasiliano kati ya vyama tawala vya nchi hizo. Yu amesema hayo alipokutana na Bw. Ghandour hapa Beijing.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako