• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Luis Figo kuwania urais wa Fifa

    (GMT+08:00) 2015-01-29 13:59:14
    Nyota wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Luis Figo ametangaza nia ya kuwania kiti cha urais wa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA katika uchaguzi wa shirikisho hilo utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu. Figo ametangaza azma hiyo akitumia ukurasa wake binafsi wa mtandao wa kijamii wa Twitter ambapo aliueleza ulimwengu lengo lake la kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho kinachomhusisha rais wa sasa Sepp Blatter. Figo anakuwa mgombea wa sita kutangaza azma ya kuwania urais wa FIFA baada ya Blatter mwenyewe, mchezaji mwingine wa zamani David Ginola , makamu wa rais wa FIFA ambaye pia ni rais wa chama cha soka cha Jordan Mwanamfalme Ali Bin Al Hussein, rais wa chama cha soka cha Uholanzi Michel Van Praag, na kiongozi wa zamani wa FIFA Jerome Champagne. Figo amesema kuwa sababu inayomuongoza kuingia kwenye mbio hizo ni kuleta mabadiliko ndani ya shirikisho hilo na kupunguza kashfa zinazoendelea kulikumba shirikisho hilo. Rais wa sasa wa FIFA Sepp Blatter anawania nafasi hiyo ikiwa ni mara yake ya tano katika wakati ambao umri wake umefika miaka 78.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako