• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wakutana kwa mara ya kwanza tangu tetesi za pambano lao kuanza

    (GMT+08:00) 2015-01-29 14:00:03
    Mabondia wawili nyota Floyd Mayweather na Manny Pacquiao juzi walikutana uso kwa uso ikiwa ni mara ya kwanza kukutana katika kipindi hiki ambacho pambano lao limekuwa likitajwa sana. Mabondia hao walikutana kwenye uwanja wa American Airlines Arena ambako walikuwa wakitazama mchezo wa ligi ya mpira wa kikapu ya NBA kati ya Miami Heat na Milwaukee Bucks. Pacquaio alihudhuria mchezo huo akiwa mgeni wa kocha wa Miami Heat Erik Spoelstra na Floyd kwa upande wake amezoeleka kama shabiki mkubwa wa Miami na amekuwa akihudhuria michezo mingi ya timu hiyo. Mabondia hao walionekana wakizungumza kwa kifupi kabla ya kupeana mkono na kuagana huku kila mmoja akienda kivyake. Hivi karibuni mashabiki wa masumbwi wamekuwa wakizungumza kuhusu pambano la mabondia hao wawili na kumekuwa na mazungumzo ambayo yanaendelea japo hayajaweza kufikia hatua yoyote nzuri.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako