• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kipa wa Yanga, Juma Kaseja apandishwa kizimbani

    (GMT+08:00) 2015-01-29 14:01:00
    Kipa wa Yanga, Juma Kaseja kupitia kwa wakili wake, Samson Mbamba, juzi alisomewa shtaka lake kwa mara ya kwanza la kuvunja mkataba kwenye Mahakama ya Kazi. Kesi hiyo itanguruma tena Februari 12 na Yanga wanataka Kaseja awalipe Sh340 milioni ikiwa ni ada ya usajili, ambayo ni Sh40 milioni pamoja na fidia ya Sh300 milioni, ambazo ni gharama za usumbufu wa kuvunja mkataba, kumhudumia na kutunza kiwango chake kwa kipindi chote alichokuwa Yanga. Kaseja aliingia kwenye mgogoro na uongozi wa Yanga baada ya Novemba 11 mwaka jana, kuandika barua ya kuvunja mkataba na klabu hiyo baada ya kukiuka makubaliano ya mkataba kati yao, akishinikiza kulipwa Sh20 milioni za usajili alizokuwa anaidai klabu hiyo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako