• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Adhabu kwa wachezaji na kocha zatawala wiki hii

    (GMT+08:00) 2015-01-30 14:05:09
    Chelsea imepata pigo baada ya mshambuliaji wake Diego Costa kupigwa marufuku kucheza mechi ya kesho Jumamosi dhidi ya Manchester City kwenye Ligi Kuu England baada ya kukutwa na hatia ya kumchezea madhambi ya makusudi kiungo wa Liverpool, Emre Can wakati timu zao zilipomenayana Jumapili iliyopita kwenye nusu fainali ya Kombe la Ligi. Ukiweka kando adhabu ya mshambuliaji huyo muhimu wa Chelsea, Chama cha soka England kimemtoza pia faini ya Pauni 25,000 kocha Jose Mourinho kutokana na kauli yake kwamba kumekuwa na kampeni ya waamuzi kwa ajili ya kuiangamizi timu yake aliyowahi kuitoa Desemba 28 baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Southampton kwenye Ligi Kuu. Nchini Hispania, nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefungiwa kucheza mechi mbili baada ya kukutwa na hatia ya kumshambulia mchezaji mwenzake kwenye mechi dhidi ya Cordoba Jumamosi iliyopita. Kwenye mchezo huo, ambao Ronaldo alichemsha kwanza alimpiga ngumi usoni mchezaji Jose Crespo kabla ya kumpiga teke Edimar na kumfanya atolewe kwa kadi nyekundu. Real Madrid ilishinda 2-1, lakini Ronaldo aliomba radhi baadaye kupitia ukurasa wake wa Twitter kutokana na tukio hilo. Ronaldo atakosa mechi dhidi ya Real Sociedad na Sevilla.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako