• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  •  Van Persie akiri hayupo kwenye kiwango bora

    (GMT+08:00) 2015-01-30 14:10:43
    Nyota wa Manchester United Robin Van Persie amekiri kuwa huenda akaihama klabu hiyo pale ambapo mkataba wake utakapomalizika ndani ya kipindi cha miezi 18 ijayo. Van Persie ametoa kauli hii baada ya kujikuta akicheza chini ya kiwango kwa muda mrefu sasa ambapo ameshindwa kuonyesha ubora wake aliowahi kuwa nao kipindi alipohamia akitokea Arsenal. Van Persie amekuwa kwenye wakati mgumu kiasi cha kumfanya kocha wa klabu hiyoLouis Van Gaal kufikiria kumuacha nje ya kikosi cha kwanza na kutoa nafasi kwa wachezaji wengine wa nafasi ya ushambuliaji. Hata hivyo kiwango cha mdachi huyu kimeonekana kuanza kurejea katika hali yake ya kawaida katika michezo ya hivi karibuni ambapo ameweza kuifungia United mabao 8 tu , idadi ambayo si nzuri kwa mshambuliaji wa kiwango cha Van Persie .
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako