• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la pili la madaktari wa China nchini Liberia lapokea mgonjwa wa kwanza aliyethibitishwa kuambukizwa Ebola

    (GMT+08:00) 2015-02-02 09:39:48

    Kundi la pili la madaktari wa China nchini Liberia limepokea mgonjwa wa kwanza aliyethibitishwa kuambukizwa Ebola. Mkurugenzi wa kituo cha matibabu ya Ebola cha China nchini Liberia Zhang Yong amefahamisha kuwa, mgonjwa huyo ni mwanamke mwenye umri wa miaka 49, na jamaa yake alifariki siku 10 zilizopita kutokana na Ebola.

    Baada ya kumpokea mgonjwa huyo, kundi hilo lilianza utaratibu wa matibabu. Mkuu wa kundi hilo Yang Haiwei amesema hivi sasa hali ya mgonjwa huyo ni tulivu, na wanafanya kila wawezalo ili apone haraka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako