• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yasema jaribio kubwa la chanjo mbili za Ebola kuanza nchini Liberia

    (GMT+08:00) 2015-02-03 10:18:56

    Taasisi ya Taifa ya Afya ya Marekani imesema jaribio kubwa la kutathmini usalama na ufanisi wa chanjo mbili za Ebola limeanza jana nchini Liberia.

    Taasisi hiyo imesema jaribio hilo linaloongozwa na ushirikiano wa utafiti wa kimatibabu kati ya Liberia na Marekani, kwanza unafanyika Monrovia mji mkuu wa Liberia, kukiwa na vituo 10 vya chanjo. Jaribio hilo linalotarajiwa kukamilika Juni 2016, litajumuisha wanaume na wanawake elfu 27 wenye afya na wenye umri wa miaka 18 na zaidi. Chanjo hizo mbili zimeonekana kuwa na usalama na kuweza kuzidisha kinga inayohitajika ili kujilinda dhidi ya maambukizi, hali ambayo ilionekana wakati wa majaribio ya mwanzoni ya kundi dogo la watu wenye afya waliojitolea wa Marekani na Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako