• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa mafunzo kwa wahudumu wa afya elfu 10 wanaoshughulikia tiba ya Ebola katika nchi za Afrika magharibi

    (GMT+08:00) 2015-02-06 19:48:59

    Wataalamu wa afya wa China waliopelekwa Afrika magharibi wametoa mafunzo kwa wahudumu wa afya zaidi ya elfu 10 wanaoshughulika na tiba dhidi ya ugonjwa wa Ebola.

    Gazeti la Health News linalomilikiwa na Kamati ya Afya na Uzazi wa Mpango ya China limesema, tangu Novemba 4 mwaka jana, China imepeleka madaktari bingwa 64 wa Ebola ambao wametoa mafunzo kwa madaktari, manesi na wahudumu wa afya za umma katika nchi za Sierra Leone, Liberia, Guinea na nchi nyingine sita katika kanda hiyo ikiwemo Senegal.

    Hii ni mara ya kwanza kwa China kutoa mafunzo ya afya katika nchi za nje, hatua ambayo imeiwezesha China kutoa elimu na uzoefu iliyopata katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa SARS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako