Viongozi wa ligi ya La Liga Real Madrid juzi Jumamosi walikiona cha mtema kuni baada ya kukandamizwa mabao 4 bila jibu na wapinzani wao Atletico Madrid katika mechi ya Derby iliochezwa katika uwanja wa Vincente Calderon. Real iliyokuwa ikiuguza majeraha mengi ililazimika kuingiza mabeki m'badala katika mechi yao ya ugenini. Hata hivyo mabeki hao hawakuweza kuhimili kishindo cha mashambulizi ya mabingwa wa ligi Atletico Madrid Mabao ya haraka yaliyofungwa na Tiago, Saul Niguez yaliiweka Atletico kifua mbele katika kipindi cha kwanza, kabla ya mabao mengine mawili yaliyofungwa katika kipindi cha pili na Antoine Griezman na Mario Mandzukic kushindilia msumari wa moto kwenye kidonda cha Real Madrid.
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |