Mapambano kati ya mashabiki wa soka na vikosi vya usalama mjini Cairo, Misri, yamesababisha vifo vya takriban watu 22. Mapambano hayo yamekuja kufuatia mashabiki wa klabu ya Zamalek kutaka kuingia uwanjani kwa nguvu bila ya tiketi katika mechi ya ligi kuu dhidi ya ENPPI. Katika vurugu hizo polisi walilazimika kutumia gesi ya machozi ili kuwatawanya mashabiki katika uwanja wa Air Defense wa Cairo, huku watu 20 wakijeruhiwa. Mwaka 2012, zaidi ya mashabiki 70 waliuawa katika vurugu zilizotokea baada ya mechi huko Port ambapo sasa Misri imewapunguzia mashabiki uwezo wa kushiriki mechi kufuatia vurugu hizo. Watu wengi wanaamini kuwa polisi wa Port wanalipiza kisasi kwa uhusika wa mashabiki katika machafuko ya kupinga kupinduliwa Mubarak. Polisi imekanusha shutuma hizo.
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |