• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazisaidia nchi zinazoathiriwa na Ebola kuanzisha na kuboresha mfumo wa afya ya umma

    (GMT+08:00) 2015-02-09 16:55:11

    Naibu mkurugenzi wa Kamati ya Afya na Uzazi wa Mpango ya China Bw. Ma Xiaowei amesema China inazisaidia nchi zinazoathiriwa na Ebola kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huu na kuanzisha na kuboresha mfumo wa afya ya umma wa nchi hizo. Vilevile Bw. Ma amefahamisha kuwa, hakuna tukio la maambukizi ya Ebola, wala watu wanaodhaniwa kuambukizwa virusi vya Ebola nchini China kwa sasa.

    Kauli ya ofisa huyo imekuja kutokana na uvumi kuwa kuna mtu mmoja ameambukziwa ugonjwa wa Ebola katika sehemu ya kaskazini nchini China. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na ofisi ya habari ya Baraza la serikali la China, Bw. Ma Xiaowei anasema:

    "hakuna mtu yeyote aliyeambukizwa ugonjwa wa Ebola nchini China, wala mtu anayedhaniwa kuambukizwa. Sasa tunajumuisha nguvu mbalimbali na kutekeleza jukumu letu, ili kusaidia kudhibiti maambukizi ya Ebola Afrika magharibi, na kuzisaidia nchi husika kuanzisha na kuboresha mfumo wa afya ya umma wa nchi hizo."

    Takwimu zinaonesha kuwa ili kusaidia Afrika magharibi kupambana na maambukizi ya Ebola, China imetoa misaada yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 120, na kuwatuma wahudumu wa afya na wataalamu wa afya ya umma karibu 800 kwa ujumla kwenye nchi zilizokumbwa na Ebola.

    Habari zaidi zinasema kikundi cha upimaji cha maabara inayotembea cha China nchini Sierra Leone kimepima damu ya watu karibu 4,000, na kuwatibu watu zaidi ya 600. Na kituo cha matibabu ya Ebola cha China nchini Liberia kilianza kazi tarehe 25 Novemba mwaka jana, mpaka sasa kimepokea watu zaidi ya 100, na kuwatibu wagonjwa zaidi ya 60.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako