• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkurugenzi wa UNDP afanya ukaguzi kuhusu hali ya ugonjwa wa Ebola nchini Liberia

    (GMT+08:00) 2015-02-17 09:55:16

    Mkurugenzi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa Bi. Helen Clark ametoa tahadhari kuwa, mlipuko wa ugonjwa wa Ebola hauwezi kumalizika mpaka pale kutakapokuwa hakuna mtu aliyepata maambukizi ya ugonjwa huo, wakati huohuo ameipongeza serikali ya Liberia na watu wake kwa juhudi zao za kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo.

    Nchini Sierra Leone, rais Ernest Bai Koroma wa nchi hiyo ametoa wito kwa umma kuwa wavumilivu baada ripoti iliyotolewa na Mkaguzi Mkuu wa serikali kuonyesha kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya kukabiliana na Ebola zimetumika vibaya.

    Taarifa iliyotolewa na ikulu ya nchi hiyo imeweka wazi kuwa, watakaokutwa na hatia ya kutumia fedha hizo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

    Habari nyingine zinasema, Afrika Kusini, kwa kushirikiana na Tume ya Umoja wa Afrika inayounga mkono mapambano dhidi ya Ebola katika nchi za Afrika magharibi, zinapelekea wahudumu 23 wa afya katika nchi zilizoathirika na Ebola. Wahudumu hao, wakiwemo wauguzi 20 na wasaidizi watatu wa madaktari, wanatarajiwa kuondoka mjini Johannesburg, Afrika Kusini, ijumaa wiki hii kuelekea nchini Sierra Leone.

    Nchi za Liberia, Guinea, na Sierra Leone zimeathirika zaidi na ugonjwa wa Ebola, ambapo watu zaidi ya elfu 9 wamefariki tangu ugonjwa huo ugundulike nchini Guinea mwezi Desemba mwaka 2013.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako