• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa IAAF akiri kuwa riadha inakabiliwa na mgogoro juu ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu

    (GMT+08:00) 2015-02-17 15:06:03

    Mkuu wa Shirikisho la riadha Duniani Lamine Diack amekiri kwamba michezo hiyo inakabiliwa na mgogoro juu ya madai ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu dhidi ya wanariadha wa Russia. Mwezi Disemba televisheni moja ya Dokumentari nchini Ujerumani ilidai kuwa maofisa wa Russia wanakubali malipo kutoka kwa wanariadha kusambaza dawa zilizopigwa marufuku za kuongeza nguvu halafu kuwafichia wanariadha hao wanapochukuliwa vipimo. Diack alisema alishtushwa aliposikia madai hayo kwa mara ya kwanza. Lakini rais huyo wa Shirikisho la Riadha Duniani mwenye miaka 81 kutoka Senegal amesisitiza kuwa madai ya kwamba asilimia 99 ya wanariadha wanatumia dawa za kuongeza nguvu si kweli na hayana maana, na kusema kwamba hawezi kukubali kwamba mtu atokee tu na kusema asilimia 99 ya wanariadha wa Russia wanadanganya, hilo sio sahihi kabisa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako