Bingwa wa WBC na WBA wa uzito wa welterweight Floyd Mayweather amesema anatarajia pambano lake na Manny Pacquiao litafanyika, lakini makubaliano bado hayajafikiwa. Mayweather Mmarekani mwenye miaka 37 na Pacquiao miaka 36 hivi karibuni walipena namba za simu katika mechi ya mpira wa kikapu, wawili hao wanazingatiwa kuwa mabondia wazuri sana wa sasa. Mayweather alisema kumekuwa na uvumi na uzushi mwingi lakini bado hajasaini makubaliano ila ana imani kubwa kufanyika kwa pambano. Hivi karibuni msemaji wa Pacquiao alisema pambano la mabondia hao bado lina safari ndefu sana lakini kuna matumaini kwamba huenda likafanyika. Hayo yote yamekuja baada ya ripoti kusema Pacquiao amekubali kupigana na kwamba pambano litafanyika Mei 2 huko Las Vegas.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |