• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Usain Bolt aionya Puma kutomvisha jezi za timu pinzani Arsenal

    (GMT+08:00) 2015-02-17 15:07:18

    Mkimbiaji aliyeiteka dunia katika mbio fupi, Usain Bolt wa Jamaica ambaye anajulikana kwa mapenzi yake kwa mabingwa wa zamani wa England, Manchester United, ameionya Kampuni ya Puma ambayo inamdhamini, kuachana na wazo la kumvalisha jezi ya klabu ya Arsenal ambayo pia inadhaminiwa na kampuni hiyo, kwa madai kwamba hawezi kuvaa jezi ya adui. Bingwa huyo wa dunia wa mbio za mita 100 na 200 amekuwa akidhaminiwa na Puma tangu mwaka 2003, huku Arsenal ikiwa imeanza kuvaa jezi za Puma katika msimu huu huku wakilipwa dau la Pauni milioni 30 kwa mwaka katika mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya Pauni 150 milioni. Hata hivyo, licha ya mapenzi yake kwa Kampuni ya Puma, Bolt amedai kwamba hakuna kiasi chochote cha pesa ambacho kinaweza kumfanya aisaliti timu yake Manchester United kwa kuvaa jezi ya Arsenal japo kwa tangazo la biashara tu. Mkiambiaji huyo ambaye ametangaza kustaafu mbio kuanzia mwaka 2017 baada ya michuano ya dunia, ameeleza vile vile jinsi asivyoielewa staili ya soka ya kocha wao wa sasa hivi, Louis van Gaal. Bolt anaamini kama angeamua kuwa mwanasoka, mchezo ambao anaupenda sana, angependa kucheza kama winga wa upande wa kushoto na kukimbiza mabeki wa timu pinzani kwa kasi kubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako