• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Manchester United kuvaana na Arsenal robo fainali ya kombe la FA

    (GMT+08:00) 2015-02-18 09:26:19

    Hatimaye timu nane zitakazocheza robo fainali za Kombe la FA huko England zimejulikana baada ya kukamilika kwa michezo ya kufuzu kucheza hatua hiyo. Mabingwa watetezi wa kombe la FA, Arsenal watapambana na Manchester United katika hatua hiyo ya nane bora. Arsenal watasafiri kwenda Old Trafford kuikabili Manachester United katika mchezo wa robo fainali zitakazochezwa tarehe 7 au 8 ya mwezi Machi. Manchester United ilijihakikishia nafasi hiyo ya hatua ya nane bora baada ya kuishindilia Preston North End mabao 3-1. Mpambano kati ya Arsenal na Manchester United unatajwa kuwa mkali katika robo fainali hiyo. Liverpool itakuwa mwenyeji wa Blackburn, Bradford City itapambana na Reading wakati wapinzani wa jadi kutoka West Midlands Aston Villa na West Brom zitamenyana katika uwanja wa Villa Park. Hatua ya robo fainali kwa timu ya Liverpool itampa matumaini nahodha wake Steven Gerrard kucheza fainali katika uwanja wa Wembley ukiwa ni msimu wake wa mwisho kuwa katika kikosi cha Liverpool, japokuwa watatakiwa kuishinda Blackburn ambao tayari waliwatoa nje ya kinyang'anyiro cha kombe la FA Swansea na Stoke timu za ligi kuu ya England msimu huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako