Mwenyekiti wa Shirikisho la Riadha la Russia Valentin Balakhnichev ameacha kazi baada ya kashfa ya hivi karibuni kuhusu wanariadha kutumia dawa za kuongeza nguvu. Uamuzi wa kiongozi huyo umekuja mwezi mmoja baada ya wanamichezo watano wakiwemo mabingwa watatu wa Olimpiki kupigwa marufuku na kocha Valentin Maslakov kujiuzulu. Kwa sasa makamu wa mwenyekiti Vadim Zelichenok atachukua nafasi yake hadi uchaguzi utakapofanyika ndani ya miezi sita ya olimpiki ya Olimpiki ya mwaka 2016. Mwezi Disemba chaneli ya Das Erste ilionesha Dokumentari nchini Ujerumani ikidai kuwa maofisa wa Russia wanakubali malipo kutoka kwa wanariadha kusambaza dawa zilizopigwa marufuku za kuongeza nguvu halafu kuwafichia wanariadha hao wanapochukuliwa vipimo. Wakti huohuo siku ya Jumatatu rais wa Shirikisho la Riadha Duniani Diack alisema alishtushwa aliposikia madai hayo kwa mara ya kwanza, Lakini kusisitiza kuwa madai ya kwamba asilimia 99 ya wanariadha wanatumia dawa za kuongeza nguvu si ya kweli na hayana maana.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |