Morocco imekata rufaa kwenye Mahakama ya Usuluhishi ya michezo baada ya kupigwa marufuku kushiriki mashindano mawili yajayo ya kombe la mataifa ya Afrika. Nchi hiyo ilipigwa marufuku kushiriki michuano ya mwaka 2017 na 2019 kwa kushindwa kuandaa michuano ya mwaka huu. Morocco pia imetozwa faini ya dola milioni 1 na kuamuriwa kulipa dola milioni 9 kama fidia ya kujitoa katika dakika za mwisho kuandaa michuano hiyo kwa kuhofia kuenea kwa ugonjwa wa Ebola. Mapema mwezi huu Shirikisho la Soka la Morocco limesema linakataa vikwazo vyote vya soka na pesa vilivyowekwa dhidi yao. Hivyo limeamua kuipeleka kesi hiyo kwenye mahakama ya usuluhishi iliyopo Uswizi, na kuomba adhabu walizopewa zitenguliwe hadi kufikia mwishoni mwa mwezi ujao. Shirikisho hilo limesisitiza hawana ugomvi na CAF, isipokua wamefanya hivyo kwasababu sheria inaruhusu na watakubali maamuzi yoyote yatakayotolewa na mahakama.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |