• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baada ya mashambilizi mengi sasa van Gaal ataka kununua kiungo

    (GMT+08:00) 2015-02-18 09:28:16

    Baada ya kushambuliwa na vyombo vya habari vya Hispania, makocha na wachambuzi soka, kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amekiri kwamba anataka kununua kiungo mwishoni mwa msimu. Van Gaal amelalamikiwa na watu wengi kutokana na kitendo chake cha kumchezesha mshambuliaji Wayne Rooney kama kiungo wa kati, lakini sasa amedai kwamba anatafuta mtu wa kucheza nafasi hiyo. Hata hivyo, Van Gaal amesema Rooney (29), ambaye hajafunga bao lolote katika mechi tisa zilizopita, hana tatizo lolote la kucheza kama kiungo na akakiri kwamba staa huyo anajua watu wanazungumza nini kuhusu nafasi yake mpya uwanjani. Rooney alianza msimu kama mshambuliaji wa mbele na kufunga mabao manane katika mechi 14, hivyo kuwa mfungaji wa tatu bora wa muda wote Old Trafford kabla ya kurudishwa kucheza kiungo. Bao lake la mwisho alifunga Desemba 26 mwaka jana katika ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Newcastle na alicheza kama mshambuliaji. Mara ya mwisho kwa Rooney kucheza kwa muda mrefu bila ya kufunga ilikuwa kati ya Desemba 2005 hadi Februari 2006. Hata hivyo, kauli ya Van Gaal kuhusu kukitia nguvu kikosi cha United, inaweza isipokelewe vyema katika bodi ya timu hiyo baada ya kutumia kiasi cha Pauni 150 milioni katika dirisha kubwa la mwaka jana akinunua wachezaji saba na mmoja kati yao akiwa kiungo mchezeshaji Mhispaniola, Ander Herrera.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako