• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi zilizoathiriwa na Ebola zaweka mipango ya kufufua uchumi

    (GMT+08:00) 2015-02-18 09:28:18

    Marais wa Guinea, Liberia na Sierra Leone wamekutana mjini Conakry nchini Guinea kwa ajili ya mkutano kuhusu kufufua uchumi wa nchi zao na kupitisha mpango wa kufufua uchumi.

    Taarifa iliyotolewa mjini Conakry inasema marais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia, Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone na Alpha Conde wa Guinea wametumia fursa ya mkutano huo kuratibu sera taratibu na nyaraka zinazohusu nchi hizo tatu, zilizoandaliwa na mawaziri wa nchi hizo. Marais hao wamepongeza mpango uliopendekezwa na Benki ya dunia wa kufufua uchumi baada ya kipindi cha ugonjwa wa Ebola.

    Marais hao pia wameitaka jumuiya ya kimataifa kutoa uungaji mkono wa moja kwa moja kwenye bajeti za nchi hizo, na kuzifutia madeni nchi zilizoathiriwa na ugonjwa wa Ebola. Vilevile wamesisitiza kuwa wataendelea kuhimiza utekelezaji wa mpango wenye lengo la kutokomeza kabisa ugonjwa wa Ebola ndani ya siku 60.

    Hali ya ugonjwa Ebola kwa ujumla inaendelea kutulia, nchini Liberia hadi sasa ni watu 6 tu wanaotajwa kuwa na ugonjwa wa Ebola. Jumuiya ya kimataifa nayo inaendelea kuzisaidia nchi zilizoathiriwa na ugonjwa huo. Benki ya dunia, shirika la kilimo na chakula la Umoja wa mataifa FAO pia wamesema watatoa dola za kimarekani milioni 5 kwa ajili ya wakulima vijijini nchini Guinea.

    Sierra Leone nayo inatarajiwa kupoteza dola za kimarekani milioni 920 kutokana madhara ya ugonjwa wa Ebola

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako