• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kupanua ujenzi wa miundo mbinu mikubwa ya usafiri

    (GMT+08:00) 2015-02-22 18:49:24

    China inapanga kupanua ujenzi wa miundo mbinu mikubwa ya usafiri katika mwaka huu kwa ajili ya kudumisha ukuaji wake wa kiuchumi.

    Kamati ya Mageuzi na Maendeleo ya China imesema njia zaidi za reli haswa katika sehemu za kati na magharibi ya China zitaanza kutumiwa mwaka huu hali ambayo itadumisha ukuaji wa kiuchumi na kuboresha maisha ya watu. Kamati hiyo imeongeza kuwa itaendelea kuhamasisha mtaji wa kijamii kupitia njia zinazofaa kuwekeza kwenye sekta ya miundo mbinu mikubwa ya usafiri mwaka wa 2015.

    Hivi sasa China ina zaidi ya kilomita 110,000 za njia ya reli ambapo kati ya hizo elfu 15,800 ni za reli ya kasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako