Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF limesema wapiganaji wasiojulikana wamewateka nyara watoto 89 katika mji wa Malakal, kwenye jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini.
UNICEF imesema, wapiganaji hao walikusanyika nje ya eneo la makazi ya watu, na kuanza msako wa nyumba kwa nyumba na kuwateka nyara watoto, ambao wengi wao ni wa zaidi ya miaka 12.
Mjumbe wa shirika hilo nchini Sudan Kusini Bw. Jonathan Fitch amesema, kitendo hicho cha kuwateka nyara watoto kinakwenda kinyume na sheria ya kimataifa. Amesema kitendo cha kuwateka nyara watoto na kuwalazimisha washiriki kwenye mapigano kinasambaratisha familia na jamii kwa jumla.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |