Dereva wa timu ya Mclaren Fernando Alonso ametoka hospitali baada kupata ahueni kufuatia ajali iliyomkumba. Bigwa huyu wa dunia mara mbili amerudi nchini Hispania kujiunga na familia yake kwa ajili ya mapumziko na kuweza kupona kabisa. Majeruhi haya ya Alonso yatasabaisha kukosa kwa raundi ya tatu ya majaribio ya magari yatakayofanyika kuanzia leo huko Barcelona. Timu ya Mclaren imesema dereva Kevin Magnussen atashirikiana na Jenson Button katika kujaribu magari. Timu za magari yaendayo kasi zinajiandaa kuanza msimu mpya utakaoanza Machi 15.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |