Waziri wa michezo nchini Misri, Khaled Abdel-Aziz amesema nchi yake imetupilia mbali jitihada za kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mwaka 2017 ambapo mbali na uamuzi wao wa kujiondoa wameahidi kuiunga mkono Algeria. Shirikisho la Soka Afrika linatarajia kutoa jina la wenyeji wa michuano hiyo mwezi April ambapo Libya nayo ilikuwa miongoni mwa nchi hizo lakini ilijiondoa kutokana na hali ya kisiasa inayoendelea nchini humo. Waziri Khaled amesema Misri haitaweza kushindana na Algeria wataunganisha nguvu kushirikiana ili Algeria ishinde nafasi hiyo. Hali si shwari upande wa Misri baada ya kutokea vifo vya mashabiki 22 mwezi Februari wakati Polisi walipokuwa wakipambana na mashabiki kabla ya mchezo kati ya Zamalek na ENPPI, na kupelekea shughuli za soka kusimamishwaa, hata hivyo kwa sasa imetangazwa kuwa ligi nchini humo itaanza tena mwezi Machi lakini bila ya ushiriki wa mashabiki. Pia haikuwekwa wazi tarehe gani itaanza ligi hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |