Mkongwe wa soka duniani David Beckham amedhihirisha kuwa alitumia vyema nafasi yake akiwa uwanjani na kujenga jina na heshima kwenye soka ambayo itamfanya akumbukwe duniani. Beckham ambaye alizichezea klabu za Manchester United na Real Madrid jana alitangazwa kuwa, ukongwe wake na heshima aliyoiacha kwenye soka vinawafanya watu wanaoandaa tuzo za HMV Football Extravaganza nchini Uingereza kusema kwamba kwenye sherehe hiyo mwaka huu tuzo hiyo rasmi itatolewa kwa David Beckham. Tuzo hii ni ishara ya kuutambua mchango wa Beckham kwenye soka duniani. Beckham mwenyewe ameipokea kwa furaha taarifa hii kwa kuwa kwenye orodha ya nyota wachache waliobahatika kupewa tuzo hiyo akiwemo Sir Alex Fergusson na Kocha Jose Mourinho. Maadhimisho ya miaka 20 ya Tuzo za HMV Football Extravaganza yatafanyika September 1 mwaka huu ambapo Beckham atakabidhiwa tuzo yake pamoja na kufanyika harambee ya kuchangisha pesa ambazo zitakwenda kwenye taasisi ya Nordoff Robbins kwa ajili ya kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali ya kiafya na kijamii Uingereza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |