• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FIFA kutotoa fidia kwa klabu yoyote ya Ulaya kufuatia kombe la dunia kufanyika mwishoni mwaka 2022

    (GMT+08:00) 2015-02-26 14:46:48

    Shirikisho la Soka Duniani FIFA, limetangaza kuwa halitazilipa fidia klabu zozote za soka barani Ulaya ambazo hazijafurahia hatua ya FIFA kuandaa kombe la dunia nchini Qatar mwezi Novemba na Disemba ya mwaka 2022. Katibu mkuu wa shirikisho hilo, Jerome Valcke, amesema FIFA haina haja ya msamaha wowote wa maandalizi ya uwenyeji wa mashindano hayo, ambayo yanatazamia kutatiza kwa kiasi kikubwa ratiba ya michuano ya ligi kuu barani Ulaya. Mapendekezo ya jopo la FIFA yalisema kuwa mashindano ya kombe hilo la dunia nchini Qatar yatafanyika wakati wa baridi ili kuepuka msimu wa kiangazi katika mataifa ya ghuba ambayo hushuhudia joto kali mno. Valcke pia amesema kombe la mataifa ya Afrika AFCON la mwaka 2023 litaahirishwa kutoka Januari na kufanyika mwezi Juni ili kusaidia kufanyika kwa kombe hilo la dunia, na Shirikisho la Soka la Afrika CAF limeshakubali kubadilisha tarehe ya michuano yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako