• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya na nchi za Afrika kufanya mkutano kuhusu ufufuaji wa uchumi baada ya Ebola

    (GMT+08:00) 2015-02-27 09:58:56

    Umoja wa Ulaya umezialika nchi za Afrika kwenye mkutano wa ngazi ya juu mjini Brussels, ili kupitia maendeleo ya juhudi za kupambana na ugonjwa wa Ebola na kuweka mpango wa kuisaidia Liberia na nchi nyingine za Afrika kurudi katika hali ya kawaida baada ya kukumbwa na Ebola.

    Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Ulaya inasema marais na mawaziri wa Guinea, Sierra Leone na Togo, na maofisa wa Umoja wa mataifa, Jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS na Umoja wa Ulaya watahudhuria mkutano huo.

    Katika mkutano huo utakaoendeshwa chini ya uenyekiti wa pamoja wa Rais Ellen Johnson Sirleaf, mpango wa 11 wa mfuko wa maendeleo wa Umoja wa Ulaya wa mwaka 2014 hadi 2020 kwa ajili ya Liberia utasainiwa na Liberia na Umoja wa Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako