Bomu la vita vya pili vya dunia ambalo halijalipuka limepatikana karibu na uwanja wa Borussia Dotmund wa Signal Iduna. Bomu hilo lililoripotiwa na mwandishi wa DW nchini Ujerumani kuwa ni la Uingereza limepatikana jana na sasa kuna mpango wa kulivunja makali. Ugunduzi huo umetokea saa kadhaa kabla ya mkufunzi wa klabu hiyo Jurgen Klopp kuzungumza na vyombo vya habari kabla ya mechi ya siku ya Jumamosi dhidi ya klabu ya Shalke. Watu waliokuwa karibu na uwanja huo unaobeba takriban watu 80,720 waliondolewa. Wamiliki wa kilabu hiyo waliofunga eneo la mashabiki pamoja na makumbusho ya klabu hiyo wamesema haijulikani ni kwa muda gani eneo hilo la uwanja litakuwa haliendeki.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |