• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mchezaji wa Serbia Zarko Udovicic atishiwa kwa bunduki na mashabiki wa klabu baada ya kukosa penalti

    (GMT+08:00) 2015-02-27 14:53:20

    Mchezaji wa Serbia Zarko Udovicic ametishiwa kwa mtutu wa bunduki na mashabiki wa timu yao baada ya kukosa penalti. Mlinzi huyo wa Novi Pazar alipiga penalti kwenye mlingoti wa goli katika mechi kali ya Serbia dhidi ya FK Rad iliyochezwa wiki iliyopita. Siku mbili baadaye, watu kadhaa walivamia kwenye chumba cha kubadilishia nguo kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo huku akielekezewa mtutu wa bunduki usoni mwake. Tangu hapo mchezaji huyo ameripotiwa kuondoka kwenye klabu yake. kisanga hicho kilichotokea katika dakika ya 85 na kupelekea FK Rad kushinda mechi kwa goli 1-0. Rais wa chama cha wachezaji soka wataalamu cha Nezavisnost, Mirko Poledica amesema si Shirikisho la Soka la Serbia wala ligi waliochukua hatua dhidi ya kitendo hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako