• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Licha ya ajali Fernando Alonso kushiriki msimu mpya wa mbio za magari

    (GMT+08:00) 2015-02-27 14:54:00

    Boss wa timu ya magari yaendayo kasi ya Mclaren Ron Dennis amesema dereva Fernando Alonso anatarajiwa kushiriki msimu mpya wa mbio za magari za Grand Prix zitakazo fanyika Australia. Kwa sasa Alonso mwenye miaka 33 yuko nchini kwao Hispania kwa mapumziko baada ya kupata ajali. Dennis amesema uamuzi wa mwisho kama Alonso ataweza kushiriki michuano hiyo utatolewa na madaktari japo anaendelea vizuri kabisa. Alonso hatoweza kushiriki majaribio ya Magari yanayofanyika huko Barcelona na kumpelekea dereva Dane Kevin Magnussen kuwa dereva mwenza wa Jenson Button katika timu hiyo Mclaren.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako