• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Arsenal yagaragazwa vibaya nyumbani na AS Monaco

    (GMT+08:00) 2015-02-27 14:54:53

    Matumaini ya Arsenal kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Ulaya yameingia kasoro hapo juzi baada ya kukubali kipigo nyumbani na kupata aibu kubwa mbele ya mashabiki wao baada ya kuchapwa mabao 3-1 na AS Monaco ya Ufaransa katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mabao ya Geoffrey Kondogbia, Dimitar Berbatov na Yannick Ferreira-Carrasco yalitosha kwa Monaco kupata ushindi wao maarufu kabisa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya Arsenal. Goli la kufutia machozi la Arsenal limefungwa na Oxlade Chamberlain. Arsenal iliyoonekana kumiliki mpira kwenye kipindi cha kwanza na hata cha pili, ilishindwa kutumia nafasi zao na mabadiliko ya kocha Arsene Wenger kwa kuwatoa Francis Coquelin, Olivier Giroud na Santi Cazorla na kuwaingiza Theo Walcott, Alex Oxlade-Chamberlain na Tomas Rosicky kilionekana kuwapa nguvu Arsenal na kupata bao moja la kujifariji kupitia kwa Chamberlain. Mchezo huo uliokuwa wa kwanza kwa kocha Wenger kukutana na klabu yake ya zamani katika mechi za mashindano baada ya miaka 20 kupita na kwamba kikosi chake cha Arsenal sasa kipo kwenye wakati mgumu katika mchezo wa marudiano utakaofanyika mjini Monaco mwezi ujao. Katika mechi nyingine ya michuano hiyo Bayern Leverkusen ya Ujerumani ilipata ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Atletico Madrid. Goli hilo pekee la Bayern Liverkusen lilitiwa kimiani na Hakan Calhanoglu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako