Wachezaji wawili wa Tanzania wa mchezo wa tenisi kwa wachezaji wenye ulemavu wapo nchini Kenya kuiwakilisha nchi yao katika michuano ya Afrika ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia kwa vilabu la BNP (BNP Paribas World Team Cup African Qualification tournament) yanayofanyika jijini Nairobi, Kenya. Kenya, ikiwa nchi mwenyeji imezikaribisha nchi za Afrika Kusini, Tanzania, Ghana, Morocco na Mauritius katika michuano iliyoanza jana Nairobi na kumalizika siku ya Jumapili. Washindi watafuzu kucheza michuano ya timu ya dunia (BNP Paribas World Team Cup) itakayofanyika klabu ya Alibey Manavgat, nchini Uturuki kuanzia May 25 mpaka 31. Kwa mujibu wa viongozi wa Chama cha Tenisi Tanzania (TTA), wachezaji kutoka Tanzania ni Novatus Temba na Emmanuel Masapinib wakiwa chini ya kocha Riziki Salum.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |