• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wapitisha azimio la kuadhimisha miaka 70 ya kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia

    (GMT+08:00) 2015-02-27 18:44:33

    Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 ya kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, na kutoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kutosahau waliojitoa muhanga na vitendo vya kikatili wakati wa vita hiyo.

    Azimio hilo limepitishwa katika kikao cha 69 cha baraza hilo lenye nchi wanachama 193. Azimio hilo linasisitiza kuwa "vita hiyo ni tukio la kihistoria ambalo lililotoa msingi wa kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, kuzuia vita katika siku za baadaye, na kuepusha vizazi vijavyo kuathiriwa na vita kama hiyo.

    Wakati huohuo, mwenyekiti wa zamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu ambaye pia ni balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Liu Jieyi amesema, azimio hilo lina maana kubwa ya kihistoria na umuhimu mkubwa kwa sasa. Amesema China inatumai nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa zitafanya juhudi kujenga dunia yenye amani na masikilizano, kama inavyoelekezwa kwenye Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako