• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chelsea wawa wafalme wa kombe la Capital One

    (GMT+08:00) 2015-03-02 14:20:15

    Klabu ya soka ya Chelsea imetawazwa kuwa mabingwa wapya wa kombe la Capital one baada ya kuicharaza mabao 2-0, timu ya Tottenham katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Wembley Jumapili jioni. Katika mechi hiyo vijana wa kocha mwenye maneno mengi Jose Mourinho waliandika bao la kwanza katika dakika ya 45 ya mchezo huo kupitia nahodha wake John Terry, bao hilo lilidumu mpaka timu hizo zilipokwenda mapumziko. Katika kuzidisha mambo yawe mabaya zaidi dakika ya 56 mlinzi wa Tottenham Kyle Walker aliwahakikishia vijana wa darajani ushindi mkubwa baada ya kujifunga katika harakati za kuokoa hatari kwenye lango lake. Kombe hili ni la kwanza kwa kocha Mourinho tangu ajiunge kwa mara nyingine klabuni hapo mwaka 2013 akitokea nchini Hispania alikokuwa akiifundisha miamba ya soka nchini humo Real Madrid.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako