• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Robin van Persie arejea tena kupata majeraha mara kwa mara

    (GMT+08:00) 2015-03-02 14:20:40

    Robin van Persie amerejea tena kupata majeraha mara kwa mara na sasa atalikosa pambano la FA dhidi ya Arsenal litakalosakatwa Machi 8 viwanjani Old Trafford wakati timu yake Manchester United itakapokuwa nyumbani. Mdachi huyo anatazamiwa kuwa nje kwa mwezi mzima baada ya kuumia kifundo cha mguu katika pambano dhidi ya Swansea City walilochapwa mabao 2-1 uwanjani Liberty Jumamosi iliyopita. Majeraha ya Van Persie yamekuja katika wakati mgumu kwa Van Gaal ambaye kikosi chake kimekuwa kikipigana kufa na kupona ili kurudi katika nafasi za kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Mashetani Wekundu hao wana mechi nne za Ligi Kuu England mwezi huu Mechi zikiwamo mbili dhidi ya Tottenham na Liverpool ambao ni wapinzani wao wa moja kwa moja katika kuwania nafasi nne za juu ili kutinga Ligi ya Mabingwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako