Mchezaji mkongwe wa Arsenal, Thiery Henry amefichua kuwa ndoto yake kuu ni kumrithi kocha wa timu hiyo Arsene Wenger katika klabu hiyo. Mchezaji huyo wa zamani ambaye ndiye anayeongoza kwa idadi ya mabao katika klabu hiyo akiwa na magoli 228, aliripotiwa kupewa nafasi ya kuanza kufundisha soka katika chuo cha ukufunzi wa soka katika klabu hiyo mapema mwezi uliopita. Raia huyo wa ufaransa amekiri kwamba ana mipango ya kumrithi Wenger wakati kocha huyo atakapoamua kustaafu. Baada ya kuhojiwa Henry alisema hajui ni kwa muda gani Wenger anataka kuendelea kuwa kocha wa Arsenal, lakini ni muhimu kwanza awe mzoefu wa kutosha kuchukua wadhifa huo, aidha amesisitiza kwamba kuwa kocha wa Arsenal ni ndoto yake kubwa, lakini kwanza anafaa kujifunza, na hicho ndio kitu muhimu,
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |