Baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo yasiyo ya kuridhisha katika ligi kuu ya England tangu kuanza kwa mwaka 2015, klabu ya Manchester United juzi jumamosi iliwakaribisha Sunderland kwenye uwanja wao wa nyumbani. Mchezo huo wa raundi ya pili ya EPL, umemalizika huku kikosi cha Louis van Gaal kikipata ushindi wa magoli 2-0. Wayne Rooney alifunga magoli yote mawili na kuweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya ligi hiyo kufunga magoli zaidi ya 10 katika misimu 11 mfululizo. Rooney alifunga alipiga mkwaju wa penalti baada ya mshambuliaji Radamel Falcao kuchezewa vibaya na kusababisha kutolewa kwa Wes Brown badala ya John Oshea aliyecheza vibaya licha ya pingamizi kutoka kwa mashabiki. Manchester united iliongeza bao la pili baada ya Rooney kufunga kwa kichwa baada ya mkwaju wa Adnan Januzaj kupanguliwa na kipa. Ushindi huo umeimarisha harakati za kilabu hiyo kuwania nafasi nne bora katika ligi hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |