• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Azam Fc ya Tanzania yaaga mashindano ya Ligi ya mabingwa Afrika

    (GMT+08:00) 2015-03-02 14:22:25

    Azam Fc imeaga mashindano ya Ligi ya mabingwa Afrika baada ya kufungwa mabao 3-0 katika mchezo wa marudiano wa mzunguko wa awali uliofanyika Uwanja wa Marreikh mjini Khartoum. Merreikh ilimaliza dakika 45 za kwanza ikiwa inaongoza bao 1-0 huku kipindi cha pili ikafanikiwa kushinda mabao mawili zaidi yaliyofungwa na Ahmed Abdallah dakika ya 85 na Allan Wanga dakika ya 90. Azam ilitolewa kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya awali kushinda 2-0 katika mchezo wa kwanza nyumbani, Uwanja wa Azam Compex, Chamazi, Dar es salaam. Kwa upande wa Yanga SC wao wanatarajia kumenyana na Klabu ya FC Platnum ya Zimbabwe katika mzunguko wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika baada Yanga kuitoa BDF XI ya Botswana. Nayo FC Platnum ya Zimbabwe, iliifumua Sofapaka FC ya Kenya na kusonga mbele kwa jumla ya magoli 4-2. FC Platnum iliilaza Sofapaka 2-1 jana kwenya mechi ya mkondo wa pili iliyosakatwa Uwanja wa Mandava Mjini Zvishavane, Zimbabwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako