• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China siku zote yatetea ushirikiano wa kimataifa

    (GMT+08:00) 2015-03-02 19:36:22

    Mkutano wa tatu wa baraza la 12 la mashauriano ya kisiasa la China utafunguliwa kesho mjini Beijing. Akizungumza na waandishi wa habari hii leo, msemaji wa mkutano huo Lu Xinhua amesema China siku zote inatetea ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na ugaidi.

    Lu amesema mpaka sasa China imeanzisha utaratibu wa ushikiano wa kupambana na ugaidi na nchi zaidi ya 10 duniani kwa kubadilishana taarifa, kusaidiana katika uchunguzi na kuimarisha uwezo wao. Aidha China imeshiriki katika utaratibu wa ushirikiano wa pande nyingi katika vita dhidi ya ugaidi, kama vile Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai na Baraza la kupambana na ugaidi duniani.

    Akizungumzia mageuzi ya kisiasa ya mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong, Lu amesema msimamo wa serikali kuu ya China kuhusu suala hilo ni wazi na usiobadilika, kwamba serikali kuu inaunga mkono Hong Kong kuendeleza demokrasia hatua kwa hatua na kwa utaratibu, na inaunga mkono watu wa Hong Kong kumchagua mkuu wa mkoa huo moja kwa moja itakapofika mwaka 2017. Amesisitiza kuwa uchaguzi huo unatakiwa kulingana na sheria ya kimsingi ya Hong Kong, maamuzi ya kamati ya kudumu ya bunge la umma la China, na hali halisi ya Hong Kong, na mkuu atakayechaguliwa lazima awe mzalendo anayeipenda Hong Kong na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako