• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa China kukua kwa asilimia 7 katika robo ya kwanza ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2015-03-02 20:25:54

    Uchumi wa China unakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 7 katika robo ya kwanza ya mwaka huu.

    Taarifa iliyotolewa na kituo cha habari cha taifa cha China imesema, kasi ya ongezeko la uchumi wa China inapungua kwa utaratibu, huku kasi ya ongezeko la uwekezaji katika soko la nyumba na sekta ya uzalishaji ikiendelea kupungua.

    Ongezeko la manunuzi linatarajiwa kuwa imara chini ya muktadha wa kuongezeka kwa mapato na kushuka kwa bei za bidhaa, huku kasi ya ongezeko la uuzaji katika nchi za nje ikiongezeka kutokana na ufufukaji wa uchumi duniani na mkakati wa "Eneo la kiuchumi la Nji Hariri na Njia Hariri Baharini" zinazochochea uwekezaji na biashara ya China katika nchi za nje.

    Lakini mahitaji ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi yanapungua kutokana na kupungua kwa soko la ndani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako