• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sikukuu ya wanawake

    (GMT+08:00) 2015-03-09 10:32:25

    P. Katika kipindi cha leo tutazungumzia matumizi salama ya kondomu. Lakini kabla ya kujadili suala hilo, ikumbukwe tu kwamba jana ilikuwa ni siku ya wanawake duniani, na kama kawaida dunia nzima ilijumuika pamoja kuadhimisha siku hii yenye kauli mbiu "Uwezeshaji Wanawake:Tekeleza Wakati ni Sasa".

    C. Pili, kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha jamii kutambua mchango wa wanawake katika kuleta maendeleo yao; na kuelimisha wadau kuangalia upya wajibu wao wa kuwashirikisha, kuwaamini na kuwapa wanawake haki sawa katika nafasi za elimu, uchumi na uongozi ili waweze kuwa chachu katika maendeleo yao.

    P. Ndio Caro kwani miongoni mwa maendeleo hayo ni kuhakikisha wanawake wanajikinga vizuri na maradhi mbalimbali na pia kuhakikisha wanakuwa na kauli wakati wa kujamiana, kwani historia inaonesha kuwa mwanamke mara nyingi huwa anaridhia tu chochote kile anachoamuriwa na mwanamume inapokuja kwenye suala la kujamiana.

    C. Kondomu inachukuliwa kuwa ni moja ya uvumbuzi 100 unaotoa athari zaidi kwa binadamu katika karne ya 20. Kwa sababu kondom inasaidia kukinga mambo mengi, mbali na maradhi lakini pia inaweza kudhibiti idadi ya watu kwa ufanisi. Na kwa upande wetu sisi wanawake, kondom ina faida kubwa zaidi kuliko njia nyingine za kuzuia mimba, ambayo inaondoa taabu nyingi na kubadilisha maisha ya wanawake wengi sana.

    P. Lakini tukiangalia kwa hali ya jumla kweli vijana wanapenda kutumia kondomu daima kwa lengo la kujilinda na maradhi na mimba zisizotarajiwa, kwa sababu vijana wengi huwa wanajisahau baadhi ya wakati, wakidhani mara moja tu hawezi kuathirika na chochote, kumbe inahitaji hiyo mara moja tu kuweza kupata ujauzito, au maradhi ya maamubuikizi. Licha ya watu kuwa na uelewa kuhusu kondomu na uwezo wake wa kuzuia magonjwa, lakini matumizi bado sio makubwa sana kwa baadhi ya watu hususan katika nchi za Afrika.

    C. Hapo amezungumzia masuala muhimu kuhusu watu kuwa na wapenzi wengi, na kuaminiana kupita kiasi, suala kubwa hapa sio kuaminiana ikija kwenye suala la kujamiiana, wanawake wanatakiwa wajiamini wao wenyewe kwa kuhakikisha kuwa kwa vyovyote vile wanatumia kondomu wakati wa kufanya tendo hilo, hapa wanaweza kutumia za kike au za kiume, isipokuwa tu wawe waangalifu na kutochanganya zote mbili kwa pamoja, kwani inakuwa rahisi kupasuka.

    P. Lakini pia kuna suala la wazazi kukaa na watoto wao kuwafahamisha matumizi salama ya kondomu, ingawa kwa mila na desturi zetu mtoto anatakiwa afundishwe yote hayo pale anapoolewa lakini kwa wakati huu tulionao tutake tusitake watoto wanaelewa na wanajamiiana kama kawaida, hivyo ni vyema kukaa na mtoto na kumuongoza ama kumfahamisha matumizi ya kondomu kwa usalama wake. Hata hivyo kwa upande wa serikali huwa zinajitahidi kuelimisha matumizi salama ya kondomu kupitia matangazo mbalimbalimbali ikilinganishwa na wazazi nyumbani, Bi Anna Stercia na Bi Janet Marwa wanafafanua jinsi serikali ya Tanzania inavyotoa uelewa kwa wananchi wake.

    C. Tumesikia jinsi serikali ya Tanzania inavyojitahidi kuelimisha vijana na watu kwa ujumla juu ya kuwa na ngono salama. Lakini mbali na Tanzania hapa China kuna mwandishi mmoja maarufu ambaye pia ni daktari na mfanyabiashara Bw. Feng Tang yeye alisema kwenye programu moja ya televisheni kuwa, kabla ya uvumbuzi wa kondom, wanawake hapa nchini China walikuwa wakikabiliwa na hali mbalimbali zinazofedhehesha na zisizoridhisha, wakijitahidi kutoa mimba isiyotarajiwa.

    "Kwa mfano baadhi ya wanawake walijipiga tumboni, walikimbia kimbia, waliruka chini na juu, walikula vyakula visivyo vya kawaida, wakaharisha, na balaa nyingi ziliwatokea. Hali zote hizi zilitajwa kwenye vitabu vya historia nchini China. Kwa hiyo kondom kwa kiasi kikubwa imeweka mazingira ya kuwakomboa wanawake, kuinua hadhi yao, na kuwafanya waweze kujiamulia."

    P. Kama tunavyosema kila siku kwenye matatizo yoyote yale wanawake ndio wanakuwa wa kwanza kuathirika, lakini kwa sasa kwa vile kuna kondomu, kadhia zote hizo zimeondoka na hii ni kutokana na wanawake wenyewe kuhakikisha kuwa hawaburuzwi au kudhibitiwa wakati wa kujamiiana. Hata hivyo suala la wazazi kutozungumzia kondomu kwa watoto wao halipo Afrika tu hata hapa China pia lipo. Bw. Feng Tang anasema:

    "Sielewi kama, wazazi hao wanawaweka watoto wao katika hali ya hatari zaidi ama la. Na pia sijui kwa nini wazazi wanaona aibu na kujiepusha kuzungumzia mambo ambayo watoto wao wameshayajua, na wangepaswa kuyajua."

    C. Analozungumzia Bw. Feng Tang ni sahihi kabisa, kwa sasa wakati umefika kwa wazazi kuwa na mwamko wa kuwa wazi kwa watoto wao, kuwaelimisha matumizi salama ya kondomu na madhara ya kutotumia kondomu kwani wahenga wanasema tusipojenga ufa tutajenga ukuta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako